Digital Marketing

Sponsored Ads” jinsi inavyoongeza Mauzo haraka kwenye biashara

3 min read

Sponsored Ads (Matangazo yaliyofadhiliwa) ni soko ambalo mtangazaji utafuta matokeo bora katika biashara au huduma anayoitoa. Inaweza kuwa njia ngumu kwa baadhi yao lakini ni muhimu sana katika kufanya kampeni yeyote inalolenga kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi na katika eneo husika. Katika jamii ya sasa Sponsored Ads ni njia mbadala ya kupata matokeo bora kwenye biashara.

Takwimu zinaonyesha Kuna zaidi ya watumiaji wa bilioni 2.01 kwenye mtandao wa Facebook kila mwezi, na kama utafanikiwa kutengeneza matangazo yaliyodhaminiwa ya Facebook (Facebook Sponsored Ads) kwa ajili ya biashara yako basi inaweza kukusaidia kufikia watazamaji wengi zaidi kupitia Idadi hiyo ya watu wanaojihusisha na mtandao wa Facebook.

Kulingana na utafiti uliofanywa na  MarketingLand, Facebook inatoa karibu 25% ya trafiki yote ya mitandao wa kijamii. Hii inamaana kuwa Facebook ina trafiki kubwa mnon kulik jukwaa lolote la Mitandao ya kijamii. Kwa hiyo, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wa kutengeneza trafiki kubwa kwenye biashara yako, tu kama utaamua kutumia Sponsored Ads kupitia Mtandao wa Facebook.

Kwa nini unapaswa kutumia matangazo ya kudhaminiwa na Facebook (Sponsored Ads)?

Kutumia Facebook Sponsored Ads kunatoa matokeo bora hasa kwenye kutangaza biashara yako au huduma yako kuliko njia nyingine yeyote. Na hii n i kwa kutokana na sababu zifuatazo,

1. Inakupa uwezo wa kutangaza biashara/huduma yako kwenye eneo husika(Location)

Unapofanya matangazo ya Sponsored, mara zote inakupa chaguzi ya kuchagua wapi unataka kuwatangazia biashara au huduma yako. Mfano unaweza kuamua kutangaza biashara kwa eneo lote la Tanzanaia pekee, au kutangaza katika eneo lote la Dar es salaam Pekee, ama Kinondoni, Ilala, Temeke na hata Ubungo peke. Pia unaweza kuamua iwe Dodoma pekee au Mwanza na hata Arusha.

Hii inakupa faida ya kuwa na wateja ambao ni walengwa kwenye biashara yako, kwa sababu watu uliowalenga wanapatika katika eneo ambalo wewe umelilenga kama eneo lako la kibiashara.

2.   kuchagua Umri wa wateja wako (Age)

Kuna baadhi ya biashara huwa zinazingatia umri wa wateja, mfano kama unafanya biashara ya vinywaji ambavyo ni vilevi, ni wazi kuwa unahitaji watu wenye umri usiopungua miaka 18. Kwa kawaida hao ndio wateja wako.

Hivyo basi kwa kutumia Facebook Sponsored Ads unaweza ukachambua umri wa wateja wako kwa urahisi ili kupata wateja halisi.

3.   Inakupa uwezo wa kuchagua Jinsia unayoilenga kuitangazia (Gender).

Zipo biashara zinazozingatia jinsia, yaani ya kike na ya kiume. Kuna biashara ambazo wateja wake maalumu ni wa jinsia ya kike lakini zipo biashara ambazo wateja wake maalum ni jinsia ya kiume.

Mfano baishara ya nguo na kadhalika zote uzingatia jinsia. Hivyo basi unapotumia Sponsored Ads inakupa uwezo wa kutangaza biashara yako kwa wateja ambao ni walengwa.

4.   Lugha (Language)

Lugha nayo ni kigezo kikubwa katika biashara. Na ndio ni njia ya mawasiliano kwenye biashara yeyote. Unapofanya matangazo ya biashara yeyote kwanza lazima ujue nani unamlenga kwenye baishara yako. Hivyo basi kwa kufanya hivyo utakuwa katika upande ulio salama katika kuchagua lugha ambayo itawapa ujumbe halisi na kwa haraka zaidi.

Unapoamua kutumia Facebook Sponsored Ads, itakupa chaguzi ya lugha ambayo ndio njia pekee ya mawasiliano baina yako na mteja wako. Ikiwa hakuna mawasiliano mazuri basi inaweza kuwa kizuizi katika ufanyaji wa biashara yako. 

5.   Inaleta watu wenye interest moja pamoja

Facebook Sponored Ads, inashirikisha watu wenye lengo moja na interest moja. Mara nyingi tunafanya baishara kwa kuangalia mahitaji ya wateja au eneo husika. Mfano, inaleta pamoja watu wenye interest mbalimbali kama vile michezo, mbalimbali kama mpira wa miguu, kuogelea, mbio za magari lakini hata watu wenye kupendelea kufanya mambo fulani kama vile kucheza muziki, kuvaa mavazi yenye kupendeza n.k.

Hivyo basi njia hii ni muhimu sana katika kukuza na kuongeza mauzo kwenye biashara mbalimbali, kwa sababu inamlenga moja kwa moja mlaji wa biashara au huduma unayoitoa. 

Ili kuweza kuingia kwenye mfumo huu na kuwa miongoni mwa watu ambao wananufaika kwa kujitangaza katika mfumo huu ambao ni rahisi na gharama yake ni ndogo mno, Jifunze hapa RodLine Academy


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *